Sh.milioni 600 zatolewa kurusha Nbc Championship

 

DAR ES SALAAM: Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amevitaka vilabu shiriki vya Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) kutumia fursa ya Ligi hiyo kuoneshwa mubashara kwa kujitangaza ili kushawishi wadhamini.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya uingiaji mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Sh Milioni 613, kati ya TFF na kituo cha TV3 kwaajili kuonesha mubashara  NBC Championship.

“Ligi ya NBC Championship itakapokuwa inarushwa na TV3 na TV3 Sports, dunia itashuhudia ligi ngumu katika ukanda wa Afrika,” amesema Karia

Rais huyo amesema, hatua zinazopigwa katika mpira wa miguu ni kutokana na mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kushawishi wawekezaji zaidi.

Aidha, Msimamizi wa vipindi wa TV3, Emmanuel Sikawa amesema wanaenda kuonesha zaidi ya michezo 170 ya NBC Championship kupitia TV3 na TV3 Sports watakayoizindua siku za usoni.

“Tunatambua waliopita walifanya vizuri lakini sisi tutaenda kuendelea pale walipoishia na kwenye mapungufu tutasahihisha ili kuwa bora zaidi,” amesema Sikawa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments