DAR ES SALAAM: Afya ya mlinda lango wa Simba ya Dar es Salaam na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Aisha Manula ‘Tanzania One’ inaelezwa kuimarika.
Hii ni kwa mujibu wa picha mnato zilizorushwa na mitandao rasmi ya kijamii ya klabu yake.
“Air Manula ndani ya Mo Simba Arena kwa mara ya kwanza tangu alipopata majeraha” Simba imedokeza.
Itakumbukwa, taarifa iliyochapishwa na tovuti ya Simba mnamo Mei 29, 2023 ilidokeza kuwa Tanzania One amesafiri kwenda Afrika Kusini kwaajili ya matibabu ya nyama za paja.
Hali iliyomfanya Manula kukosa michezo ya mwisho ya msimu wa 2022/23 sambamba na mechi za michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAFCL).
0 Comments