SIMBACHAWENE ATOA MAAGIZO TASAF

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameagiza kusitishwa kwa fedha zinazotolewa kwa walengwa wasio na sifa wa Mpango wa kunusuru Kaya maskini nchini (Tasaf) na badala yake fedha hizo zipangiwe kazi nyingine.


Akizungumza leo Septemba 13, 2023 baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mpango huo kwa mkoa wa Geita,Waziri Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa na waratibu wa Tasafa kusitisha malipo pindi tu wanapobaini mlengwa aliyeingizwa kimakosa kwenye mpango huo.

Akizungumzia changamoto ya utapeli unaofanywa na ndugu wa walengwa au watoa huduma za simu(mawakala) kwa wazee wakati wa malipo ya fedha zinazotolewa na Tasaf kwa mfumo wa mitandao ya simu, Waziri Simbachawene ameitaka Tasaf kuangalia namna mpya ya kuwalipa wazee ili kumaliza changamoto hiyo.

Amesema Mpango wa Tasaf kipindi cha pili awamu ya tatu ulikuja na ubunifu wa kutoa malipo kwa simu ili kupunguza gharama za uendeshaji lakini kumekuwa na changamoto ya fedha hizo kutowafikia walengwa na wasiojiweza kutokana na wao kutokua na ubunifu au uwezo wa kutumia simu.

“Tuangalie upya namna tunavyowalipa hawa wazee ili tuwaondolee hii changamoto ya kuibiwa najua mna mifumo yenu wakati mkitaka kuiboresha basi angalieni njia bora itakayowawezesha wapate fedha hizi”

Waziri Simbachawene amesema kwa kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu fedha nyingi zimetolewa  ambapo kwa mkoa wa Geita pekee zaidi ya Sh100 bilioni zimetolewa na Tasaf ambazo zimetumika kwenye ujenzi wa miundombinu ya sekta ya elimu na afya,kulipa wazee na wasiojiweza  pamoja na wale wanaotekeleza ajira za muda kwenye .

Awali, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Mipango na uratibu Deodatus Kayango amesema Tasaf kw amkoa wa Geita inahudumia kaya 46,749 zenye walengwa 220,666 ambapo kwa kipindi cha pili cha awamu ya tatu zaidi ya Sh 35.4 milioni zimelipwa kwa walengwa.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2021-2023 Mkoa wa Geita ulipokea Sh 8.09 bilioni kwa ajili ya miradi ya kuondoa umaskini ambayo ni ujenzi w amiundombinu ya elimu,Afya,miradi ya ajira za muda pamoja na miradi ya vikundi kwa walengwa.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana kupitia mpango wa Tasaf, Kayango amesema mpango huo umewezesha wananfunzi wa msingi na sekondari kupata mahitajiya watoto kwa ajili ya kuendelea na masomo.

Mafanikio mengine ni walengwa kumudu kupata mahitaji ya msingi ikiwemo ikiwemo kumudu kupata milo miwili kwa siku kutoka kwenye mlo mmoja waliokuwa wakipata awali pamoja na kufanikiwa kuezeka nyumba kwa bati kutoka nyumba za nyasi zilizokuwepo.

Pamoja na mafanikio hayo amesema bado zipo changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya walengwa hususan wazee na walemavu kutopokea fedha zao ipasavyo kutokana na wao kuwatumia watu wengine.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments