UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA WANAOHUDUMIWA NA MTAMBO WA RUVU JUU

 


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 24 * kwa siku ya *Jumamosi Septemba 16, 2023 hadi Jumapili Septemba 17, 2023.

Sababu: Kuruhusu matengenezo kwenye miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji ambayo yatasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji.

Maeneo yatakayoathirika ni;

Ruvu darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Pichandege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Msigani, Maramba mawili, Tabata, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti,Ubungo, Kisarawe, Ukonga, Pugu, Uwanja wa ndege, Majumba sita , Kiwalani na Gongo la Mboto na Kisarawe

Tafadhali kumbuka kuhifadhi maji ili kuweza kuyatumia kipindi cha matengenezo.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja

0800110064 (bure) au

0735 202 121(WhatsApp tu)




Imetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments