Recent-Post

Unyanyasaji wamuondoa Antony Brazil

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Antony Matheus dos Santos ‘Antony’ ameondolewa kwenye kikosi cha Brazil kinachojiandaa na michezo ya Kombe la Dunia dhidi ya Bolivia na Peru kufuatia madai ya unyanyasaji dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake.

Shirikisho la soka nchini Brazil (CBF) limesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya chombo cha habari nchini humo UOL kuchapisha taarifa za madai ya aliyekuwa mpenzi wa Antony, Gabriela Cavallin akimtuhumu kushambuliwa kimwili.

“Ili kumlinda mwathiriwa anayedaiwa, mchezaji timu ya taifa ya Brazil na Antony anaondolewa kwenye kikosi,” CBF ilisema.

Anthony ,23, alikanusha madai hayo kwenye mitandao ya kijamii akisema hakutoa maelezo zaidi kutokana na uchunguzi wa polisi

Post a Comment

0 Comments