DIRISHA la usajili barani Ulaya limefungwa usiku wa kuamkia leo.
Zifuatazo ni sajili zilizokamilika dakika za mwisho kabla ya kufika saa 6 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Kiungo Mason Greenwood wa Manchester United amejiunga na Getafe ya Hispania kwa mkopo, mara baada ya msimu huu kuisha atarejea Old Trafford.
United imeamua kufanya hivyo ili kumrejesha kwenye kiwango chake baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akikabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake, hata hivyo mashtaka hayo yalifutwa miezi mitatu iliyopita.
Manchester United imekamilisha usajili wa kiungo Sofyan Amrabat kutoka Fiorentina.
“Mimi ni mtu ambaye nasikiliza nafsi yangu inachokitaka, na sasa naiwakikisha klabu ya ndoto zangu.” amesema Amrabat baada ya kukamilisha usajili huo.
Kiungo Ibrahim Sangare raia wa Ivory Coast amejiunga na Notts Forest kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 35 akitokea PSV. Notts pia imekamilisha usajili wa mkopo wa mshambuliaji Divock Orig.
PSG imemsajili mshambuliaji wa Ufaransa, Randall Kolo Muani kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 90, pauni milioni 75 za uhamisho na nyongeza ya pauni milioni 15 ‘add ons’ akitokea Frankfurt.
Mkataba wa miaka mitatu imempa ulaji beki Rob Holding aliyesajili na Crystal Palace akitokea Arsenal, kwa uhamisho wa pauni milioni 4.
Beki Joao Cancelo amejiunga na Barcelona kwa mkopo akitokea Manchester City, baada ya msimu kuisha atarejea Etihad.
Brennan Johnson amejiunga na Spurs akitokea Notts Forest kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 47. Johnson amesaini mkataba wa miaka sita.
0 Comments