WABUNGE WA AFRIKA WAKUTANA KUJADILI MIFUMO BORA YA CHAKULA BARANI AFRIKA

 Wabunge 19 kutoka nchi 8 za Afrika wamekutana Jijini Dar es Salaam kwa Lengo la kujadili namna bora ya kuboresha mifumo ya kilimo, na usalama wa chakula kwenye nchi za Afrika ikiwa ni jitihada za kuondokana na utegemezi wa chakula kutoka nchi za nje.


Akizungumza kwa niaba ya Bunge la Tanzania, Mariam Mzuzuri ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya haki elimu, Mifugo Viwanda na Biashara amesema nijambo jema sana kwa nchi za Afrika kuungana ili kuwekeza nguvu ya pamoja kwenye kuboresha mifumo ya chakula Afrika kwa sababa bara la Afrika lina ardhi kubwa ambayo inaweza kutumika kwa kila aina ya uzalishaji wa chakula na kuondokana na uagizaji wa chakula kutoka nje ya nchi

Bi Mzuzuri ameongeza kuwa Tanzania ikichukua hatua kila siku ili kuinua mifumo ya kilimo nchini amabapo katika miaka miwili iliyopita ya bajeti kumekua na ongezeko la asilimia Zaidi ya 100 ili kukidhi mahitaji ya secta hiyo mhimu Zaidi nchini

Mkutano huo pia umelenga kuongeza muunganiko wa sera na fursa za pamoja kwa nchi za Africa ili kuweza kuanzisha mfumo utakaotumika kukabiliana na changamoto zinazolikumba bara la Africa kiasi cha kushindwa kuzalisha chakula kutosha kukkidhi mahitaji ya watu wake

Nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikikumbana na changamoto ya ukosefu wa chakula kwasababu ya kukosa mifumo sahihi ya usalama na udhalishaji wa chakula, hivyo muungano wa wabunge hawa watakwenda kuishauri serikali yale ambayo tumeafikia ili kuleta mabadiliko chanya katika mifumo yetu-Amehitimisha Bi Mzuzuri.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments