Wakulima Magu kunufaika na mradi kuboresha ardhi

ZAIDI ya wakulima 7000 kutoka Wilaya ya Magu mkoani Mwanza wanatarajia kunufaika na mradi wa kuboresha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD).

Hayo yamesemwa leo na mratibu wa kitaifa wa mradi huo hapa nchini, Joseph Kihaule alipotembelea miradi mbalimbali katika vijiji vya Lumeji na Nya’hanga .

Amesema mradi huo ulianza 2017 na unatarajia kumalizika 2024 na lengo kuu ni kurejesha ardhi iliyoharibika kwa mabadiliko ya tabianchi.

Amesema mradi huo una ufadhili wa Sh bilioni 1.5. Amesema mradi huo utasaidia wakulima katika kilimo,ufugaji pamoja na ujasiriamali.

Amesema mradi huo utakabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kutoa mashamba darasa kuhusu mbinu za kilimo,uvunaji wa misitu pamoja na uvunaji wa maji kupitia visima.

Amesema mpaka sasa wanufaika wameweza kunufaika na mradi wa visima katika kijiji cha Mwabayanda pamoja na mradi wa ufugaji wa kondoo katika kijiji cha Lumeji.

Naye makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo ya Klimo(IFAD) Donal Brown amepongeza maendeleo ya mradi huo wilayani Magu. Ameahidi shirika lao litaongeza miradi mingine katika wilaya hiyo ili wakazi wa wilaya hiyo waendelee kunufaika zaidi.

Mkazi wa kijiji cha Nya’hanga Henericus Kitambale amesema mradi wa maji wa visima wa Mwabayanda umewasaidia kuepuka tatizo la kwenda umbali mrefu wa kuchota maji. Amesema kabla ya mradi kufika katika kijiji chao walikuwa wanachota maji katika mto Simiyu ambapo ni mwendo wa kilomita 3.

Amesema kupitia mradi huo wameweza kuanzisha kilimo cha mpunga pamoja na kilimo cha matikiti maji na mpaka sasa ameshauza matikiti maji tani tatu.

Naye ofisa kilimo wa Wilaya ya Magu, Mussa Kiwanuka amesema katika mradi wa ufugaji kondoo katika kijiji cha Lumeji walianza na kondoo 60 na mpaka sasa kuna kondoo 90.

Amesema wakazi wa Lumeji wameweza kupata mbolea ya samadi kupitia kondoo hao. Amesema mbolea hiyo wakulima wanapeleka katika mashamba yao ili kuongeza tija ya kilimo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments