Wazazi Wakunwa Na Vipaji Shule Ya East Africa

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, akizungumza kwenye mahafali ya shule ya Awali na Msingi ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma mwishoni mwa wiki.

KATIKA kukimarisha afya ya a kili na mwili kwa wanafunzi shule ya Awali na Msingi ya East Africa iliyoko Kikuyu jijini Dodoma, imeanzisha somo la mchezo wa karate.


Mwalimu mkuu wa shule hiyo Evarist Runiba, alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya darasa la saba ya shule hiyo.

Alisema michezo hiyo ni sehemu ya kuwasaidia kuimarisha afya za wanafunzi wao ili kufanya vizuri katika masomo yao na shunguli mbalimbali za kila siku.

“Shule yetu pamoja na kufundisha masomo mengine lakini pia tunafundisha lunga ya kichina na kifaransa lakin pia tunalo darasa la mchezo wa karate ambalo wanafnzi wote wanapata mafunzo wakiwa hapa shule”alisema

Alisema katika amchezo huo wa karate wanao walimu waliobobea katika mchezo huo hali ambayo itasaidia wanafunzi hao kuwa timamu kimwili na kiakili ili kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao.

Mgeni rasmi Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, alisema amefurahishwa na vipaji mbalimbali alivyoona kwenye shule hiyo.

Alisema ni vyema shule zingine ziige mfano huo kwa kutenga muda mzuri wa wanafunzi kucheza na kuimba.

Aidha, alisema kuna wanafunzi wenye vipaji mbalimbali kama vilivyoonekana kwenye mahafali hayo na kwamba kama vipaji hivyo vikiendelezwa wanaweza kupatikana wasanii wakubwa nchini.

“Mnafanya vizuri sana na muendelee hivyo hivyo kwenye michezo na burudani kwasababu hawa wameonyesha vipaji vya aina yake natoa wito kwa shule zingine ziige,” alisema

Aidha, alisema michezo inawafanya wanafunzi wanakuwa na afya njema hali ambayo pia itachangia kufanya vizuri kwenye masomo na mitihani yao pia hivyo walimu wasione kama michezo ni kupoteza muda bila sababu.

“Mbalina masomo ya kawaida wapeni muda wa kucheza kuonyesha vipaji vyao, hawa lazima wapate muda wa kufanya mambo mengine yanayowapa furaha kama michezo,” alisema

Wanafunzi hao walionyesha umahiri mkubwa kwenye kuimba na kucheza nyimbo mbalimbali hali ambayo iliwafurahisha wageni na wazazi waliofika kwenye mahafali hayo ambapo wengine walikuwa wakiwatunza.


Baadhi ya wahitimu wa shule ya awali na Msingi ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma wakiwa kwenye mahafali yao yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa shule ya awali na msingi East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma mwishoni mwa wiki
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa shule ya awali na msingi East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma mwishoni mwa wiki
 Mkurugenzi wa shule za St Marys na East Africa ya Kikuyu Dodoma, Dk. Rose Lwakatare akizungumza kwenye mahafali ya shule ya awani na msingi East Africa Dodoma yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments