WAZIRI MKUU AWAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA MICHEZO

 WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka wananchi kwenye maeneo mbalimbali nchini washiriki katika michezo kwa kuwa michezo ni ajira, uchumi na huimarisha afya.

Tunapa faida nyingi kwa kufanya michezo, tushiriki katika michezo pamoja na kukimbia riadha kwa kuongeza vipaji tulivyonavyo kwani tukishindana tunapata na zawadi. Michezo ni uchumi.  

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumamosi, Septemba 9, 2023) baada ya kuzindua Ruangwa Marathon katika kiwanja cha Kilimahewa, wilayani Ruangwa Lindi.

Aidha, Waziri Mkuu amesema amemshukuru Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa aliyoyafanya katika sekta ya afya nchini ikiwemo na wilaya ya Ruangwa.

Amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika maeneo ya kutolea huduma za afya kwa kujenga zahanati, vituo vya afyfa na hospitali ya wilaya ambayo inavifaa tiba vya kisasa.

Mbio hizo za hisani ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza wilayani Ruangwa zimehudhuriwa na wanariadha mbalimbali wanaoliwakilisha Taifa katika mashindano ya mbio za kimataifa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Molel amesema mbio hizo za marathon ni nzuri kwa sababu mazoezi yanasaidia katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Dkt. Molel amemshukuru Waziri Mkuu kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika mbio hizo za hisani zilizokuwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kununulia vifaa tiba wilayani Ruangwa.

Pia, Dkt. Molel ameishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za afya ambapo kwasasa asilimia 97 ya wagonjwa waliokuwa wanapelekwa nje ya nchi kwa matibabu wanatibiwa nchini.

 

Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa (kushoto kwake) wakishiriki katika mbio za Ruangwa Marathon kwa ajili ya kuchangia vifaa tiba zilizofanyika Ruangwa, Septemba 9, 2023. Kulia kwake ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro na kushoto ni Mkurugenzi wa Wasafi Media, Nasib Abdul maarufu Diamond Platnum. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akizungumza katika mbio za Ruangwa Marathon zilizofanyika mjini Ruangwa, Septemba 9, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments