Bashungwa akagua ujenzi Bugene-Beneco

KAGERA: WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa serikali itahakikisha inamlipa kwa wakati Mkandarasi M/s China Road and Bridge Cooperation anayejenga barabara ya Bugene – Kasulo (Beneco) – Kamunazi (km 128.5) kwa kiwango cha lami sehemu ya Bugene – Burigi Chato yenye urefu wa kilometa 60.

Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyaishozi mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kulipa kwa wakati madai mengine yatakayowasilishwa na mkandarasi huyo, ili aweze kuongeza kasi ya ujenzi pamoja na kulipa fidia kiasi cha Sh bilioni 2 kwa wananchi waliopisha ujenzi wa barabara hiyo.

“Kuhusu fidia naomba niwaambie, mtupe kama mwezi mmoja kuanzia hii leo, tutakuwa tumekamilisha na hizo Sh bilioni 2.074 zitakuwa zimeshakuja ndani ya Wilaya ya Karagwe na wale ambao mmesubiri kwa muda mrefu tunaenda kuweka historia,” amesema Bashungwa.

Bashungwa amewataka wananchi wa Kata ya Nyaishozi kujipanga na kuhakikisha wanaweka mipango miji vizuri kwani Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, inaleta maendeleo kupitia miundombinu ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwenda nchi za jirani.

Aidha, Bashungwa wakati akikagua eneo la mlima kihanga, kuangalia changamato zinazowapata watumiaji wa vyombo vya moto katika mlima huo na kuahidi kuwa wizara itafanya haraka kutatua changamoto katika eneo hilo.

Ametoa wito kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto kuheshimu tahadhari na onyo ambazo zinatolewa kwenye vibao ambavyo vimewekwa barabarani kwani vimewekwa ili kulinda na kusaidia usalama barabarani.

“Umahiri wa dereva sio kukimbia sana kutoka sehemu moja kwenda nyingine, bali ni kuhakikisha abiria waliopo kwenye chomba chake wapo salama, hivyo pamoja na marekebisho ambayo sio suluhisho kwa asilimia 100 bado madereva wanatakiwa kuhakikisha wanazingatia masuala ya usalama barabarani ikiwemo kuacha tabia ya mwendo kasi, “ ameongeza Bashungwa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments