WAKULIMA LIMENI MASOKO YAPO ASEMA RAIS SAMIA

Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi wa Wilaya ya Mkalama kulima kwa juhudi kwani Serikali imetengeneza mazingira mazuri kwa umwagiliaji na kutoa pembejeo.

Kuhusu masoko, kiongozi huyo amesema Serikali hailali katika kuhakikisha wanapata masoko ya mazao yao yanakuwa ni ya uhakika.

Amiri Jeshi Mkuu amesema hayo Oktoba 16, 2023 wakati akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida.

“Kwahiyo niwahakikishieni limeni masoko yapo, kama soko la nje halipo kwa wakati huo serikali itanunua yale mliyozalisha,” Amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewataka wananchi kila mmoja kwa nafasi yake kufanya kazi kwa juhudi ili kupelekea maendeleo yake na taifa kwa ujumla.

Pia, Rais amewataka wananchi hususani wa mabondeni kukaa kwa tahadhari kutokana na matarajio ya uwepo wa mvua kubwa za El-Nino kuanzia mwezi huu.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa wakati wakivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Wilayani Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023 

Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria tukio la ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Wilayani Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na viongozi mara baada ya kufungua Daraja la Msingi lililopo Wilayani Mkalama katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023.

Shamrashamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika eneo la Mkutano wa hadhara pembezoni mwa Daraja la Msingi, Wilayani Mkalama katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023Taswira ya Daraja la Msingi lenye urefu wa Mita 100, lililopo katika Kijiji cha Msingi, Mkalama Mkoani Singida. Daraja hilo limezinduliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 16 Oktoba, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments