Gamondi aita mashabiki kuiua Azam

 


DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa YANGA SC, Miguel Gamondi amesema kikosi chake kipo imara kuvaana na matajiri wa Chamazi, Azam FC hapo kesho katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Gamondi amesema hayo leo Oktoba 22, 2023 jijini Dar es Salaam, katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo amesema wamejipanga kuibuka na ushindi katika mchezo huo, huku akiomba mashabiki wa Yanga kuja kwa wingi uwanjani.

“Sisemi kuwa mashabiki wa Yanga watajaza uwanja ila nina uhakika watakuja kwa idadi kubwa kuipa nguvu klabu yao. Kwetu Amerika ya Kusini, mashabiki uwanjani ni mchezaji wa 12.” Ametamatisha hivyo Gamondi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments