DSM: OFISA Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Imani Kajula amesema uwepo wa michuano ya African football League (AFL) una manufaa makubwa kwa taifa kutokana na fursa mbalimbali zitazopatikana kupitia michuano hiyo.
Kajula amesema Tanzania inapaswa kujivunia kuwa mwenyeji wa uzinduzi wa AFL.
“Licha ya kwamba ni tukio la siku moja, ila lina faida kubwa sana, kuna watu watatoka maeneo mbalimbali, kuna watakaotoka mikoani kwahiyo hiyo itakuwa pia fursa kwa wanaotaka kusafirisha mashabiki kuja Dar es salaam”amesema Kajula
Ameyasema hayo leo Oktoba 11, 2023 Dar es salaam alipokuwa akizungumzia maandalizi ya Simba kuelekea katika uzinduzi wa michuano hiyo mipya ya soka Afrika ambayo itazinduliwa Oktoba 20, 2023 Simba ikivaana na Mabingwa wa Afrika Al Ahly ya Misri.
0 Comments