Mashauri 333 yamalizwa nje ya mahakama


TANGA: Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imefanikiwa kumaliza jumla ya mashauri 333 nje ya Mahakama katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu

Hayo yamesemwa Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Dk Boniphace Luhande wakati wa ufunguzi wa baraza la pili la wafanyakazi wa ofisi hiyo lililofanyika jijini Tanga

Amesema kuwa utaratibu wa mashauri kabla ya kuyafikisha mahakamani umesaidia kupunguza wingi wa mashauri kwenye mahakama, lakini na kupunguza muda wa kuendesha madai hayo.

Amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2022/23, ofisi hiyo imeokoa zaidi ya Sh Bil 609.3, ambazo zingelipwa kwa wadaawa, endapo serikali ingeshindwa kwenye mashauri mbalimbali.

Naye Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo, Mark Mulwambo amesema kuwa baraza hilo limekuwa kiungo muhimu cha ushirikiano na uhusiano mzuri kazini baina yake na wafanyakazi.

“Malengo makuu ya mwaka huu licha ya kuiwakilisha serikali na taasisi zake katika mashauri ya ndani na nje ya nchi ni kuhakikisha tunakuwa na watumishi wenye kufanya kazi kwa ufanisi na weledi mkubwa,”amesema Mulwambo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments