MWENYEKITI CCM MKOA SINGIDA AITAKA KATAA YA TUNTU WILAYANI IKUNGI KUMALIZA MIGOGORO NA TOFAUTI ZILIZOPO

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida MARTHA MLATA ameitaka Kata ya NTUNTU Wilaya Ikungi Kuondoa Migogoro na Tofauti zilizopo, zilizosababisha kufukuzwa kwa Wenyeviti Wanne(4) wa Vijiji wa Kata hiyo. 
MLATA alisema hayo Wilayani Ikungi akiwa katika ziara yake ya kuzungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa wilaya hiyo, ambapo alisema migogoro hautakiwi ndani ya chama, ili kukiimarisha Chama.

 Alisema viongozi wa Chama wa Wilaya hiyo ya Ikungi ni lazma wawe wamoja ili waweze kusimamia Miradi ya maendeleo inayoletwa na serikali.

 Hata hivyo aliwataka viongozi na wananchi kuhakikisha wanasimama imara kumtetea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pale inapotokea baadhi ya Watu wanamsema vibaya Rais.

 Nao baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida walioambatana na Mwenyekiti huyo kwenye ziara hiyo, walisema viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM ni lazma wawatumikie wananchi ipasavyo.

                               

                               

YOHANA MSITA ambaye pia ni MNEC wa Mkoa wa Singida alisema kuwa Chama cha Mapinduzi hakitamvumilia kiongozi yeyote aliyewekwa madaraka na CCM kama atakuwa anakiuka Taratibu za Chama na Serikali.
DENIS NYIRAHA ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida alisema kuwa lengo la chama cha Mapinduzi CCM ni kushinda chaguzi zote zitakazofanyika nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ALLY MWANGA ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza Miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Ikungi.

                             MWANGA alisema kuwa kupitia Mradi hiyo inayotekelezwa na serikali imesaidia kupunguza changamoto za wananchi kufuata huduma za kijamii mbali na maeneo yao

                                                                                         

             
Na Mwandishi Wetu Raful Kinala ,Picha Na Chambua Singida.
 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments