RAIS SAMIA AFUNGUA SHULE YA MSINGI IMBELE PAMOJA NA MABWENI YA MADARASA YA SHULE YA SEKONDARI MWANAMWEMA SHEIN MKOANI SINGIDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa kuashiria ufunguzi wa Shule ya Msingi Imbele, mabweni ya madarasa ya Shule ya Sekondari Mwanamwema Shein kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Manispaa ya Singida Mjini tarehe 15 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Shule ya Msingi Imbele mara baada ya hafla ya ufunguzi Mkoani Singida tarehe 15 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mara baada ya kukagua moja ya Darasa la Shule ya Msingi Imbele wakati wa ziara yake Mkoani Singida tarehe 15 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiimba pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Imbele mara baada ya kuwasili Shuleni hapo kwa ajili ya ufunguzi wakati wa ziara yake Mkoani Singida tarehe 15 Oktoba, 2023.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Imbele wakiimba mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwasili Shuleni hapo Mkoani Singida tarehe 15 Oktoba, 2023.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments