Rais Samia ataka mabadiliko Singida.

 RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi na wananchi mkoani Singida kuhakikisha wanaendelea na kampeni ya mabadiliko ya tabia watu na kuanza kutumia vizuri fursa zilizopo katika Mkoa huo ili waweze kufaidika.

Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Singida, Rais Samia amesema wana Singida wanapaswa kujitathmini kwanini kiwango cha maendeleo ya Mkoa huo yanakuwa duni licha ya ukweli kuwa unakabiliwa na changamoto za asili kama mabadiliko ya tabianchi kwa hupokea kiwango kidogo cha mvua kwa mwaka lakini wamezungukwa na fursa na rasilimali kadha wa kadha.

Amezitaja fursa za kilimo, madini, ufugaji nyuki na miradi ya mabwawa ya kuhifadhi maji kama nyenzo ambazo zinapaswa kutumika ili kupelekea maendeleo.

“Tuwaelekeze na kuwafundisha wananchi kupanda mazao yanayostahamili ukame, pia zao la korosho linakubali katika Mkoa wa Singida,” amesema Rais Samia.

Ziara yake mkoani Singida itamalizika katika jimbo la Iramba Mashariki ambapo atazindua mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria hadi Singida.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments