RC Kagera kushughulikia wala rushwa

 


MKUU wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa amewahakikishia Wananchi wa Manispaa ya Bukoba  kuchukua hatua kwa watumishi wasio waadilifu wanaoendelea kujihusisha na rushwa na ubadhilifu wa mali za umma.

RC Mwassa alifanya mkutano wa adhara na wafanyabiashara na Wananchi katika kata ya Bilele viwanja vya soko kuu Manispaa ya Bukoba ambapo alitumia mkutano huo kutoa ufafanuzi juu ya ujenzi wa soko jipya la Manispaa ya Bukoba pamoja na stendi mpya ya kisasa ambapo amewahakikishia Wananchi kuwa kabla ya ujenzi kufanyika tayari Kuna viasharia vingi vya rushwa vimeonekana.

Baadhi ya Wananchi walisimama na kumuuliza Mkuu wa Mkoa ni  lini ujenzi wa stendi ya kisasa utaanza baada ya hivi Karibuni ujenzi kusimama katika eneo la Kyakairabwa na huku wengine wakitaka kujua je soko litavunjwa bila taarifa au watawahamisha na kuendelea na ujenzi ???

Mkuu wa Mkoa alisema kuwa serikali ilitoa Sh bilioni 1 kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa stendi mpya ,lakini badaaye serikali iliwaingiza Bukoba katika mradi mwingine unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ambao utatekeleza ujenzi wa soko na stendi ya kisasa kwa mwaka 2024/2025.

Alisema kuwa wakati anaapishwa kuja Kagera kama Mkuu wa Mkoa alimkuta mkandarasi anaendelea na maandalizi ya ujenzi wa stendi mpya bila kuwa na mchoro wala ramani ya ujenzi na ndipo akaamua kumbana mkandarasi huyo amueleze anawezaje kuanza kazi ya ujenzi bila mchoro ?! Na mkandarasi alisema ameambiwa asaini hivyo hivyo michoro itamkuta .

Alisema hata hivyo baada ya kumsimamisha mkandarasi huyo mkandarasi alisema kuwa tayari ameombwa asilimia 10 ya kazi yake kutoa kwa baadhi ya watu ambao hakuwataja majina  Kama sehemu ya shukrani ya kumpatia kazi ambapo mkandarasi huyo alitoa Sh milioni 50  na bado ajajua ni kwa jinsi gani atapata kurudishiwa fedha zake kwani kazi haufanyiki tena kwa Sasa.

“Mkandarasi aliombwa Sh milioni 50 kabla ya fedha haijaingia ,baadaye mkandarasi yule aliwabana watumishi kwamba wampe pesa ya kuanzia kazi aliambiwa angeingiziwa shilingi milioni 150 lakini akiingiziwa arejeshe milioni 50 kwao ili  waendelee kumuingizia fedha,na mkandarasi huyo alikataa akisema hataki tena kazi arejeshewe fedha aliyotoa Kama shukrani ,wakati huo hajapata mchoro, wala hana lolote anazunguka na watu wanasubiri kuitafuna Bilioni  moja ambayo ilikuwa haijaingizwa.” alisema Mwasa.

Alisema baada ya kujiridhisha kuwa utekelezaji wa ujenzi wa soko na stendi upo katika mwaka wa fedha 2024/2025 akatoa agizo kuwa Sh bilioni 1 iliyotolewa na serikali itumike kukarabati stendi ya sasa inayotumiwa na Wananchi huku akidai kuwa hakuna atakayetafuta hata sentI tano katika uongozi wake atakapokuwa mkoani Kagera hivyo wananchi wasubiri matokeo makubwa zaidi.

Akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa soko jipya alisema kuwa lazima utaratibu wa kuwaamisha wafanyabiashara utafanyika   kwanza na Baada ya ujenzi watarejeshewa maeneo Yao hivyo vikao vya kuanza kuwahakiki na maeneo yao vitaanza hivi karibuni na hakuna atakayevunja soko bila taarifa.

Aliwataka Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika maswala yote ya kuchangia Kodi ,usafi wa mji na kuendelea kuipenda serikali kwani serikali inafanya mambo makubwa kwa ajili yao na wale wanaowaza kutafuna mali za umma wataendelea kuadhibiwa kisheria.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments