Robertinho apiga hesabu za mbali zaidi

 

DAR ES SALAAM; Kocha wa Simba Roberto Oliviera ‘Robertinho’, amesema timu yake inacheza kwa malengo ndio maana anazingatia zaidi matokeo uwanjani kuliko kile watu wanachohoji kuhusu timu hiyo.

Robertinho amesema lengo la timu hiyo ni kutwaa ubingwa wa michuano iliyo mbele yao, ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara na atawatumia wachezaji ambao anaamini watamsadia kufikia malengo yake na ya timu kwa ujumla.

Kocha huyo ameyasema hayo leo Oktoba 27, 2023 Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia maandalizi ya kuikabili Ihefu kesho, na kusema licha ya kuwa na kikosi kipana hawezi kuwa na mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake kuelekea mchezo huo, ili kutoharibu muunganiko wa timu yake.

“Kuna uwezekano kesho nikaanza na baadhi ya maangizo mapya kwenye kikosi au wakaingia kipindi cha pili, kwa sasa tunaingalia michezo hii miwili iliyo mbele yetu, tukianza na kesho dhidi ya Ihefu, halafu tutaungalia mchezo wa Novemba 5 dhidi ya Yanga,” amesema.

Naye kocha wa Ihefu Moses Basena ,amesema licha ya kuwa na timu kwa muda mchache vijana wake wapo tayari kwa mchezo lakini wanatambua ubora wa Simba.

“Tunafahamu kwamba Simba imeshinda michezo yake ya ligi kwa asilimia 100, lakini pia ni timu yenye wastani mzuri wa kufunga, nimefanyia kazi baadhi ya maeneo yaliyokuwa na mapungufu na tupo tayari kupambana” amesema Basena. Mchezo huo utapigwa kesho Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments