RPC Mbeya awataka wanafunzi kufichua uhalifu

 


KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga amewataka wanafunzi mkoani humo kutokaa kimya dhidi ya vitendo vya uhalifu.

RPC Kuzaga ametoa maelekezo hayo alipotembelea shule ya msingi Azimio iliyopo mkoani humo ambapo ametoa elimu kwa wanafunzi wa darasa la nne kuhusiana na masuala ulinzi na usalama.

Kamanda huyo amewasisitizia wanafunzi hao kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu kwa walimu, wazazi na jeshi la polisi ili hatua za haraka zichukuliwe.

Akizungumza na wanafunzi hao leo Oktoba 24, 2023 kamanda Kuzaga amewataka kujiepusha na makundi yasiyofaa na badala yake wajikite katika masomo kwa kuhakikisha wana somo kwa bidii na kufaulu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments