Saka aondolewa England

 


MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Bukayo Saka ameondolewa kwenye kikosi cha England kinachojiandaa kufuzu mashindano ya Euro dhidi ya Australia na Italia kutokana na majeraha.

Saka alikosa ushindi wa 1-0 wa timu yake dhidi ya Manchester City Jumapili kutokana na jeraha la misuli ya paja.

Shirikisho la soka England ‘FA’ limethibitisha nyota huyo kuondolewa baada ya kufanyiwa uchunguzi na timu ya madaktari ya Uingereza.

England itamenyana na Australia tarehe 13 Oktoba, kabla ya kukutana na Italia katika mechi ya kufuzu kwa Euro siku nne baadaye.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments