Samia: Ahsante Kikwete kwa utumishi wako

“Ahsante kwa utumishi wako kwa umma wa zaidi ya miaka 50 kwenye Chama Cha Mapinduzi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, na baadaye kama Rais wa nchi yetu.” Ameandika Rais Samia kwenye ukurasa wake wa X akimtakia heri siku ya kuzaliwa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Kikwete aliyewahi kuwa Rais wa awamu ya nne anasherehekea siku ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 73.

“Nakutakia afya njema na wakati mwema unapokumbuka siku hii.” Ameongeza Rais Samia.

Post a Comment

0 Comments