San Marino wapata bao baada ya miaka miwili

UNAAMBIWA kwa mara ya kwanza ndani ya miaka miwili, timu ya taifa ya San Marino imefunga bao kwenye michuano rasmi, licha ya kupoteza mabao 2-1 dhidi ya Denmark kwenye mchezo wa kufuzu Euro uliopigwa usiku wa leo.

Mshambuliaji wa Manchester United, Rasmus Hojlund, ndiye aliyeifungia Denmark timu iliyofuzu nusu fainali ya Euro 2020.

Lakini Alessandro Golinucci alisawazisha katika dakika ya 61, na kuamsha shangwe kali kutoka kwa mashabiki wa Marino.

‘Minnows’ San Marino hawakuweza kushikilia bomba, dakika ya 70 Yussuf Poulsen aliipa ushindi wa bao la pili Denmark na kufuzu Euro 2024.

Danes wanasalia nafasi ya pili katika Kundi H na wanaweza kufuzu kwa ushindi dhidi ya Slovenia katika mechi yao ijayo.

San Marino sasa wamepoteza mechi 83 kati ya 84 za kufuzu Euro, isipokuwa sare tasa dhidi ya Estonia mwaka 2014.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments