Serikali kuendelea kushirikiana na mashirika binafsi

ARUSHA: Serikali inatambua mchango unatolewa na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kukuza na kulinda haki za binadamu nchini katika kufikia azma ya kujenga uchumi shindani kwa maendeleo ya wananchi

Hayo yamesemwa na Neema Mwanga, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa ufunguzi wa kikao na mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwa ni maandalizi ya kikao cha 77 cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kitakachofanyika Oktoba 20 hadi Novemba 9 ,Jijini Arusha

Amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yanamchango mkubwa katika kukuza na kulinda haki za binadamu sanjari na kupiga hatua zaidi katika haki za wanawake na watoto.

” Mashirika haya yanatoa huduma na si biashara lakini pia tunahakikisha mnapunguza utegemezi kwani serikali iliridhia mkataba wa haki za binadamu na hadi sasa Tanzania imesajili mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi ya 8000″

Naye Nkasori Sarakikya ambaye ni Mkurugenzi Idara ya Haki za Binadamu Wizara ya Katiba na Sheria,ameongeza kuwa Tanzania inarekodi nzuri ya kulinda na kukuza haki za binadamu ikiwemo haki za wanawake na nchi zaidi ya 55 Barani Afrika zitahudhuria kikao hicho.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments