Serikali kushughulikia changamoto ya umeme kwa haraka

PWANI: Serikali imeahidi kushughulikia changamoto ya umeme iliyopo nchini kwa kasi kubwa ili tatizo hilo liweze kuisha katika kipindi kifupi kuanzia sasa.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 11, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko katika Mkutano Mkuu Maalum wa Jimbo la Chalinze wa kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2020-2025) Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani.

Dk. Biteko amesema kuwa, katika kipindi cha miezi sita inayokuja ukosefu wa umeme nchini utaisha baada ya Serikali kuweka mikakati madhubuti ya kumaliza tatizo hilo nchini. Amesema Watendaji wanafanya kazi ili watanzania wapate umeme wa kutosha.

Katika hatua nyingine, Dk. Biteko ameiagiza TANESCO kupeleka umeme katika shule ya Sekondari ya Moreto ili shule hiyo iunganishwe na umeme mapema. Aidha amechangia kompyuta 10 kwenye shule hiyo maalum kwa matumizi ya TEHAMA kuwasaidia wanafunzi.

Kuhusu Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Dk. Biteko ametumia nafasi hiyo kupongeza juhudi zinazofanywa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo ujenzi wa madarasa, zahanati na miundombinu muhimu na pia kufanya vizuri katika makusanyo ya mwaka ambapo Wilaya hiyo imekusanya Sh bilioni 15.

Kwa upande wake, Rais wa Awamu ya Nne , Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan anatoa msukumo mkubwa kwenye maendeleo ya nchi yetu na fedha hizo zinaelekezwa katika miradi mbalimbali ili kukuza uchumi wa nchi.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments