Sh Bil 5 zatengwa mradi wa mazingira Tanga

TANGA; Shirika la World vision linatarajia kutumia kiasi cha Sh Bil tano kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa uhahamsishaji wa utunzaji mazingira kwa vijana ujulikanao sauti ya vijana katika wilaya nne za Mkoa wa Tanga

Mradi huo unatarajiwa kufanyika kuanzia mwaka 2024 hadi 2027 kwenye wilaya za Kilindi, Pangani, Mkinga na Handeni

Akizungumza wakati wa hafla ya ufungaji wa mradi huo awamu ya kwanza, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amesema matokeo chanya yaliyopatikana kwenye mradi huo yatasaidia kuongeza nguvu katika udhibiti na utunzaji mazingira.

“Mradi wa Sauti ya Vijana huhusisha vijana katika shughuli za uzalishaji, uchumi na biashara na hatua hiyo inawiana na mpango wa Mheshimiwa Rais Dk Samia wa kuwawezesha vijana maarufu kama Building Better Tomorrow (BBT), “amesema RC Kindamba.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Utetezi na Uhusiano wa Umma kutoka Shirika la World vision, Dk Joseph Mayala, amesema miongoni mwa mafanikio ya mradi huo ni kuundwa kwa vikundi 38 kwenye vijiji 20 vya kata tano, vyenye vijana 1,100 walionufaika moja kwa moja na wengine 24,501 walioguswa kwa namna nyingine na mradi huo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments