SHERIA ZA UWEKEZAJI NA MISAMAHA YA KODI KWA WAWEKEZAJI MAHIRI YABORESHWA NCHINI TANZANIA


Mwenyekiti wa Bodi ya Uwekezaji Tanzania Dkt.Binilith Mahenge Amewataka wawekezaji wa Ndani Kujisajili katika Kituo cha uwekezaji Nchini TIC ili waweze kunufaika na fursa Mbalimbali Zinazotolewa na Serikali katika Uwekezaji.

Akizungumza Mara Baada ya Kutembelea Viwanda vya Kusindika Alizeti na Pamba Mkoani Singida Dkt Mahenge Amesema Serikali imetengeneza Mazingira Rafiki ya Uwekezaji Hivyo ni Wakati sasa kwa Watanzania Wote wenye nia ya Kuwekeza kutumia Fursa hiyo kupiga hatua kiuchumi.

Amesema Miongoni mwa Maeneo ambayo yameboreshwa na Serikali ni Pamoja na Sheria za uwekezaji na Misamaha ya Kodi kwa Wawekezaji Mahiri.

Viongozi wa Viwanda vya Wide Flower,Mount Meru na Bio Sustain ambavyo vimetembelewa na Mwenyekiti huyo Wameishukuru Serikali kwa Kuendelea Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji huku Wakiiomba Kuendelea kutatua changamoto ambazo zimekuwa kikwazo katika Shughuli zao kama wanavyofafanua.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments