Simba wakitaka lao hawazuiliki!

SINGIDA: SIMBA imeendeleza rekodi ya ushindi katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya leo kuifunga Singida Fountain Gate mabao 1-2 Uwanja wa Liti,mkoani Singida na kuzidi kuwapa raha mashabiki wake.

Kutokana na matokeo hayo Simba imefikisha pointi 15 na kurejea kileleni kutoka nafasi ya tatu iliyokuwa ikishikilia, ikiwa imeshinda michezo yote mitano iliyocheza hadi sasa. Mabao ya Simba yakifungwa na Saido Ntibazonkiza dakika ya 26 na Mosses Phiri dakika ya 83, wakati la Singida likifungwa na Deus Kaseke dakika ya 52.

Post a Comment

0 Comments