Simba, Yanga kupangwa kundi moja?

AFRIKA KUSINI: Wawakilishi  wa Tanzania katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba na Yanga watawafahamu wapinzani wao katika hatua ya makundi leo Oktoba 6, 2023 ambapo hafla fupi ya kupanga makundi ya ligi hiyo itafanyika nchini Afrika Kusini.

Kwa mara ya kwanza katika historia Tanzania itakuwa na timu mbili kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya Vilabu Afrika.

Kumekuwa na mchecheto kwa mashabiki wa timu zote mbili kwani kuna uwezekano timu hizo kongwe kwenye kandanda la Tanzania zikapangwa kundi moja kutokana na kigezo cha mpangilio wa ubora ambapo Simba imetupwa chungu cha pili huku Yanga ikitupwa chungu cha tatu.

Chungu cha kwanza kina wababe wa Al Ahly kutoka Misri, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Wydad Casablanca ya Morocco na Esperance ya Tunisia.

Chungu cha pili kina Simba ya Tanzania, Pyramids ya Misri, Cr Belouizdad ya Algeria na Petro Luanda ya Angola.

Yanga, Al Hilal,Tp Mazembe na Asec Memosas zinakamilisha chungu cha tatu huku cha nne kikikamilishwa na  timu za Etoile du sahel, Jwaneng Galaxy, Fc Nouadhibou ya Maurtania  na Medeama Sc.

Tupe ubashiri wako jinsi makundi yatakavyokuwa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments