Tanzania kuendeleza ushirikiano na UNDP

 

DAR ES SALAAM: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amepokea Hati za Utambulisho za mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Shigeki Komatsubara katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kupokea nakala za hati hizo, Makamba amemhakikishia Komatsubara kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na UNDP ili kusogeza mbele agenda yake ya maendeleo na hivyo kuinua maisha ya watanzania kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Amesema Tanzania na UNDP zimekuwa zikishirikiana kutekeleza mipango ya maendeleo kwa kuwa zina lengo la kuboresha maisha ya watu kupitia maeneo ya utawala wa demokrasia, ukuaji uchumi, maendeleo endelevu mazingira endelevu na uhimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri Makamba ameongeza kuwa Tanzania inathmini na kutambua jitihada za UNDP katika kukabiliana na madhara yaliyotokana na janga la UVIKO 19
Kwa upande wake Mwakilishi wa UNDP Komatsubara ameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuendeleza jitihada za UNDP nchini na kuongeza kuwa atakuwa sio tu Balozi mzuri wa Tanzania bali pia atakuwa mtangaza mazuri ya Tanzania kupitia kazi zake.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments