TET yawaita wadau kujionea kazi zake

 


PWANI: TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Kituo cha Urithi wa Ukombozi Bara la Afrika wanashiriki Tamasha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni linalofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TASUBA) mjini Bagamoyo.

Tamasha hilo limeanza jana Oktoba 26, 2023 ambapo wadau mbalimbali wameombwa kuja kutembelea katika banda la TET kwa ajili ya kuweza kuangalia machapisho mbalimbali yanayotolewa na Taasisi hiyo.

Akizungumza katika maonesho hayo, Afisa Uhusiano wa TET, Angella Msangi ameleeza kuwa, katika tamasha hilo , wadau watapata kuona vitabu vya historia vilivyoandaliwa na TET vilivyoshirikisha wataalamu bobezi katika kufundisha somo la historia kutoka Taasisi mbalimbali.

“Mje mjione mauudhui yaliyomo kwenye vitabu hivyo ambayo yamelenga kumwezesha mwanafunzi kupata umahiri wa kuijua historia ya nchi yake na ya mahusiano ya Tanzania na nchi nyingine”. Amesema Angella.

Pia, amesema mwanafunzi atapata nafasi ya kujua historia iliyo nje ya Tanzania na hasa Bara la Afrika na kufahamu masuala mbalimbali.

Amesema pia katika tamasha hilo wananchi wataweza kuona machapisho mbalimbali yanayotolewa na kufahamu kazi zinazofanywa na TET kwa ujumla.

Tamasha hilo linatarajia kumalizika Oktoba 28, 2023 ambapo washiriki mbalimbali kutoka katika taasisi za binafsi za Serikali na nje ya nchi zinaashiriki.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments