Umeme wawanyima usingizi nishati

 

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema watumishi wa wizara hiyo hawapati usingizi tangu walipopewa maagizo na Rais Samia Suluhu Hassan ya kumaliza changamoto ya upungufu wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini.

Kapinga ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2023 kwenye ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Singida.

“Ndani ya wiki hizi mbili kila asubuhi Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko anafuatilia matengenezo ya mtambo wa Ubungo II wa Megawati 43, kila asubuhi anahakikisha na kusimamia, ili ndani ya wiki mbili megawati 43 ziwe zimerudi.

“Pia tunasimamia mradi wa Bwawa la Julius Nyerere kwa weledi mkubwa mno, kwa sasa tumeshafikia asilimia 92.74 tunataka kufikia mwezi Januari tuanze majaribio ya bwawa letu ili tumalizie changamoto ya umeme,” amesema Kapinga.

Amesema tayari wamepeleka umeme vijijini kwa asilimia 90 na wanaamini kufikia mwezi Juni 2024 watakuwa wamekamilisha vijiji vilivyosalia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments