VIONGOZI KEMEENI VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi -  CCM, Mkoa wa Singida MARTHA MLATA amewataka viongozi kuhakikisha wanakemea vitendo vya Ukatili wa Kijinsia katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sehemu husika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za Kisheria.

MLATA alikemea suala hilo la ukatili Kijinsia, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa chama cha Mapinduzi - CCM mkutano Mkuu wa wilaya ya Iramba, ambapo alisema vitendo hivyo vimekuwa vikisababisha mauaji katika jamii.

Alisema ni lazima viongozi wa Chama na Serikali kushirikia kutokomeza vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa za wahalifu kwenye vyombo vya usalama ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha MLATA aliongeza kuwa, kuna baadhi ya watendaji wanawanyanyasa wananchi, kitendo ambacho Chama cha Mapinduzi hakiwezi kuwavumilia watendaji wa namna hiyo.

Hata hivyo amewataka wanaCCM na wananchi kushirikiana kwa pamoja ili kuondoa changamoto zilizopo katika jamii kwa lengo la kuleta maendeleo.

Kwa upande wake MNEC wa Mkoa wa Singida YOHANA MSITA alisema wao kama viongozi hawatakubali kuona mtu anakichafua Chama cha Mapinduzi ambacho kina dhamana ya kuisimamia serikali.

MSITA aliongeza kuwa kazi ya viongozi wa CCM ni kuhakikisha wanasimamia wajibu wao wa kuisemea Serikali na Chama katika maeneo yao kwa kusema mazuri yanayofanywa na Serikali                                         



 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments