WANA CCM TUWE WALINZI NAMBA MOJA WA MIRADI INAYOLETWA NA RAIS DR.SAMIA KWAJILI YA TAIFA NA JAMII KWA UJUMLA

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi - CCM Mkoa wa Singida MARTHA MLATA amewataka Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi Mkoa wa Singida kuhakikisha wanaitunza Miradi iliyotekelezwa kupitia Ilani ya CCM ili iweze kudumu kwa muda mrefu kutoa huduma kwa wananchi.

 

Mlata amesema hayo wilayani mkalama wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzu CCM Wilaya ya Mkalama ambapo alisema kumekuwa na uharibifu kwenye baadhi ya miradi huku viongozi na wananchi wakiwa wanaona.

 Aliseama, hivyo ni wajibu wa kila mwana CCM na wananchi kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa na serikali katika maeneo yao inalindwa ili iweze kudumu kwa muda mrefu ikitoa huduma kwa wananchi.

 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, walipata fursa ya kuzungumza na Wajumbe wa Mkutano ambapo walisema madiwani ni lazima wawasimamie watendaji kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi kwenye mikutano ya hadhara ili kuwatoa hofu wananchi.

           

Walisema (Wajumbe) pia viongozi wa CCM kuhakikisha wanasajili wanacha na kuendelea kuwakumbusha kulipa Ada kwa wakati ili kuimarisha uhai wa Chama.

           

Jasmini Kinga ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa mkaoa wa singida yeye alisisitiza kuwepo kwa mahusiano na kuaminiana wakati wa kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa uadilifu katika jamii na taifa kwa ujumla. 

                          
 
Na Mwandishi Wetu Kutoka Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments