WANAHABARI WA AFRIKA WATAKIWA KUISAIDIA AFRIKA

 Wanahabari wa Afrika wametakiwa kubadili mitazamo yao kuhusu fursa zilizopo Afrika ikiwa ni pamoja na kulisaidia bara hilo.

Akizungumza na Wanahabari kutoka nchi za Afrika wakati akifungua Mafunzo kuhusu Utangazaji kwa nchi za Afrika (Anglophone Broadcasters), leo Cairo nchini Misri, Rais wa Baraza Kuu la Usimamizi wa Vyombo vya Habari nchini humo (Supreme Council for Media Regurations), Bw. Salehe El Salhy amesema kuwa ni wakati sahihi sasa kwa Wanahabari wa Afrika kueleza fursa zilizopo katika bara hilo kwa manufaa ya vijana na Afrika kwa ujumla.

“Wanahabari tuna jukumu la kuisaidia Afrika, vyombo vya habari vinatakiwa kutangaza taswira nzuri ya bara hili pamoja na kueleza fursa zilizopo kwa manufaa ya vijana”, ameeleza Bw. Salehe.

Amefafanua kuwa Bara la Afrika limekuwa na historia ya kutawaliwa miaka ya nyuma na hivyo changamoto kadhaa zimeendelea kuwepo ikiwa ni athari za ukoloni.

Aidha, mafunzo hayo kwa Wanahabari wa Afrika yaliyoanza leo nchini humo yana lengo la kuinganisha Afrika na kutangaza mafanikio ya bara hilo ikiwemo maendeleo na raslimali zalizopo kwa ajili ya watu wa bara hilo.

Mafunzo hayo yameudhuriwa na Wanahabari kutoka nchi nane ambazo ni Tanzania, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Liberia, Malawi, Mauritius and Siera Leone.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments