Watanzania waliopo Israel kurejeshwa nchini

 


DODOMA: SERIKALI imewataka watanzania waliopo nchini Israel kuwiwa kujiandikisha katika ubalozi wa Tanzania uliopo Tel Aviv ili kurejeshwa nchini.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iiliyotolewa kwa umma na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo, jijini Dodoma.

“Kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Israel na maeneo mengine ya jirani, Serikali imeandaa mpango wa kuwarejesha nchini Watanzania waliopo nchini humo,” imedokeza taarifa hiyo ya wizara.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mawasiliano inabidi yafanyike kabla ya Oktoba 15, 2023, saa 6 usiku kupitia ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Israel, kupitia barua pepe: telaviv@nje.go.tz au namba ya simu +972533044978 na +972507650072.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments