Watoto wote kuwa na vyeti vya kuzaliwa ifikapo 2025

KIGOMA: Serikali imesema kuwa kufikia mwaka 2025 itahakikisha watoto wote chini ya miaka mitano wamesajiliwa kwenye mfumo na kuwa na vyeti vya kuzaliwa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa sheria na Katiba,Dk.Pindi Chana Katika uzinduzi wa utioaji huo wa vyeti vya kuzaliwa uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre mjini Kigoma.
Waziri Chana ametoa kauli hiyo katika uzinduzi uliohudhuriwa na idadi kubwa ya wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji na vitongoji vyake ikiwa ni siku ya kwanza ya usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano.
Waziri Pindi chana amesema kuwa Mpango huo wa usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa bure kwa watoto chini ya miaka mitano kwa wakati huu ni mpango wa serikali kuhakikisha inawajali, kuwalinda na kuwawekea mipango mbalimbali ya maendeleo yao ya baadaye.
Akizungumza kabla kumkaribisha Waziri Chana kuzindua mpango huo mkoani Kigoma Mkuu wa Wilaya Kigoma Salum Kali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kigoma,Thobias Andengenye amesema kuwa kuna jumla ya vituo 443 mkoani humo ambavyo vitatumika kutekeleza mpango huo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments