WAZIRI MHE. JENISTA ATEMBELEA BANDA LA NSSF KATIKA MAONESHO YA WIKI YA VIJANA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama ametembelea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Vijana  Mkoani Manyara ambapo amezindua Wiki hiyo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.

 Naye Meneja wa Sekta isiyo rasmi, Rehema Chuma amemueleza Waziri Jenista kuwa “NSSF imeendelea kupanua wigo kwa kuwafikia vijana wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu ili wajiunge na kuchangia kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye, mwitikio wa wanaojiunga ni mkubwa, ambapo katika vyuo vya elimu ya juu tumeweza kufikia vyuo vinane na tayari wanavyuo 1,050 wameshajiunga na mpango wa kujichangia kwa hiari”.

NSSF inashiriki maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani Babati Mkoani Manyara, kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii, kusajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, elimu kuhusu huduma za NSSF kidijitali, elimu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, uwekezaji unaofanywa na NSSF.

Matukio mbalimbali katika Picha

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments