Ajifungua mapacha wanne wa kiume.

MWANAMKE mmoja Janeth Manota(27) mkazi wa Kwamorombo jijini Arusha amejifungua mapacha wanne wakiume katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha.

Mwanamke huyo aliyejifungua Novemba 26,2023 kwa njia ya upasuaji ikiwa ni uzao wake wa pili imeelezwa ,watoto wote wana afya njema na uzito mzuri wa kilogram 1.4,1.5,1.8 na 1.9.

Akizungumza hospitalini hapo, Janeth aliishukuru hospitali hiyo kwa kumpatia huduma nzuri iliyowezesha kujifungua salama ikiwa ni uzao wake wa pili ukitanguliwa na mtoto wake wa kiume aliyemzaa  mwaka 2015.

Alisema mimba ya mapacha hao wa nne ilikuwa na changamoto kubwa ya yeye kuishiwa na damu,kuumwa mgongo na kichwa na alipumzishwa kitandani tangu mimba ikiwa na miezi minne hadi kujifungua.

Mwanamke huyo alisema licha ya kukifungua salama lakini ana hofu ya kuwalea wanaye kutokana na uwezo mdogo wa kiuchumi katika familia yake na kuwaomba watanzania kumsaidia ili aweze kuwalea vizuri ikiwemo huduma ya maziwa.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha ,Felician Mtahengerwa alisema serikali ya wilaya imeanza kuchukua hatua ya kumsaidia namna ya kulea watoto hao ikiwemo kuwakatia Bima ya Afya na wadau mbalimbali wameonesha nia ya kusaidia malezi ya wapacha hao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments