Bashungwa awakataa Wakandarasi wababaishaji

TANGA: Waziri wa ujenzi, Innocent Bashungwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kuhakikisha kuwa wakandarasi wasumbufu na wababaishaji hawapewi kazi za ujenzi wa barabara nchini kote.
Akizungumza alipokagua Barabara ya Handeni-Mafuleta Km 20 ,Bashungwa amesema ni aibu kuwa na mkandarasi msumbufu anaechelewesha kazi na bado kupewa miradi mingine hali inayochelewesha maendeleo kwa wananchi.
“Mtendaji Mkuu nakuagiza kuhakikisha mkandarasi huyu HHEG hapewi mradi mwingine wa Km 30 mpaka nitakapojiridhisha na kasi yake ya ujenzi wa Km 20 alizonazo sasa ifikapo Januari mwakani ” amesema Bashungwa.
Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohammed Besta amesema tayari TANROADS imeshawapanga mameneja wa miradi katika miradi yote 69 inayoendelea nchini
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Handeni mjini, Ruben Kwagirwa amesema kuwa miradi mbalimbali ya barabara inayoendelea mkoani Tanga ya barabara ya Mkata -Kwamsisi (Km 36), Handeni Turiani (KM 108.2), Handeni- Kiberashi- Singida, (KM434), Kiberashi- Songe (KM 33.5) na Songe -Gairo kutaufungua vizuri Mkoa wa Tanga na kuunganisha na makao makuu ya nchi Dodoma kwa njia fupi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments