‘Changamkieni fursa biashara ya hewa ukaa’

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa iliyopo katika biashara ya hewa ukaa.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Mwendeshaji Mkuu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya ADAP, Yves Huasser alipokuwa akizungumzia kuhusu kongamano kubwa linalotarajiwa kufanyika Dar es Salaam, Novemba 16, 2023 kwenye Hotel ya Hyatt Regency.

“Ni biashara nzuri ambayo inaweza kuwasaidia wananchi katika maeneo mbalimbali vijijini, lakini pia inasaidia kuboresha mazingira ambayo yanaharibiwa na mabadiliko ya tabianchi, pamoja na baaddhi ya shughuli za binadamu,” amesema Huasser.

Amesema kongamano hilo litashirikisha wadau kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Marekani na Ulaya na kwamba utakuwa mkutano mkubwa wa aina yake wenye lengo la kuwajengea uwezo pia wadau kuhusu biasshara ya hewa ukaa.

Ameishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa namna wanavyoshirikiana nao katika masuala mbalimbali kuhusu mambo ya hewa ukaa.

Naye Meneja Uendeshaji wa taasisi ya Africa Carbon Agency, Cosmas Tungaraza amesema kupitia kongamano hilo masuala mbalimbali yatazungumzwa na wadau wataelewa kwa undani zaidi kuhusu biashara ya hewa ukaa.

“Fursa ya hewa ukaa zina manufaa kwa jamii na serikali kwa ujumla, ndiyo maana tunalenga kuwajengea uwezo wataalamu kuhusu mambo haya ya biashara ya hewa ukaa na miradi mingine ya kaboni,” amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments