CHATANDA AKUTANA NA WAKANDARASI WANAWAKE NCHINI

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amekutana na Chama cha Wakandarasi wanawake Nchini  na kufanya nao Kikao katika Ofisi za UWT Makao Makuu Dodoma .


Akizungumza leo  katika Kikao hicho Mwenyekiti Chatanda amewapongeza wakandarasi hao wanawake ambao wanamuunga Mkono kwa asilimia 100  Mh Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kufanya kazi za Ujenzi mbalimbali kwenye miradi Nchini.

Mwenyekiti Chatanda amewaomba wanawake wa Chama cha wakandarasi Nchini kuendelea kumuunga Mkono Mh Rais  kwa kufanya kazi ya Ujenzi kwa weredi Mkubwa ili fedha ambazo zimeletwa katika Maeneo  tofauti ya Nchi basi yatumike kikamilifu.

Mwenyekiti Chatanda amesema najua wanawake jinsi mkipewa kazi mnavyofanya kwa weredi Mkubwa basi msiniangushe Mwanamke mwenzetu mwendeni na juhudi hiyohiyo katika kutimiza wajibu wenu wa kazi pindi mnapoaminiwa kufanya kazi sehemu mbalimbali ya Nchi yetu fanyeni kwa weredi .

"Najua Chama chenu kipo imara katika kuwasaidia wanawake wakandarasi Nchini naombeni ushirikiano mnaondelea kuutoa kwa wanawake wengine muendelee nao ili Serikali hiendelee kujua jinsi wanawake mnavyofanya kazi kubwa katika Nchi "

Hata hivyo Mwenyekiti Chatanda ametoa Rai kwa Chama hicho cha wakandarasi Nchini kuwasaidia wanawake wa chini katika kuunganisha kuingia katika Chama hicho ili waweze kujiinua kiuchumi.

Mwenyekiti Chatanda amesema sisi kama wanawake wa UWT Taifa tutawapa ushirikiano mzuri katika kufanikisha kazi zenu kwa kuwa Mh Rais anawapenda wanawake kwa kuwa nyie ndio mnaoinua uchumi wa Tanzania .
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments