DHAMIRA YA RAIS SAMIA YA KUMSAIDIA MAMA NA MTOTO YAZIDI KUJIONESHA KWA VITENDO - (MCC) CHATANDA

 Mwenyekiti Chatanda amesema Dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imezidi kujidhiirisha kwa Vitendo katika kila kona ya Nchi ya Tanzania.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda (MCC), leo alipotembelea na kujionea namna ya utoaji huduma ya Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Bahi katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Dodoma.

Akiwa Hospitalini hapo, (MCC) Chatanda alipokea changamoto ya fedha kiasi cha Tsh Milioni 228 iliyotengwa kufika hospitalini hapo lakini baadae ikarudi.

Akotolea majibu ya jitihadi zitakazofanyika kurejesha fedha hizo, (MCC) Chatanda amesema "Kama Bajeti litengwa kuletwa katika Hospitali hii na bahati mbaya fedha hizo zikarudi, basi mnipe nakala ya barua ili sasa tuongee na Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba ili kuona namna ya fedha hizo kuletwa ilikusudi kukamilisha Ujenzi wa baadhi ya Majengo ambayo hayajakamilika kwa asilimia 100% Hospitalini hapa"

Pia, (MCC) Chatanda amemtaka DMO Wilaya ya Bahi kuhakikisha wanatoa huduma ya Elimu kwa Wananchi ili kuweza kujua na kutambua huduma zinavyotolewa kulingaba na ngazi za huduma za Afya kwa maana kuanzia Zahanati, Kituo Cha Afya hadi Hospitali ili kuweza kupunguza na kuondokana na Malalamiko ya Wananchi kuwa hakuna dawa na kumbe zipo.

Naye, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Kassim Kolowa amemueleza (MCC) Chatanda mafanikio waliyonayo katika kutoa huduma za Upasuaji kwa Wamama wajawazito na wale wanaojifungua kawaida.

Dkt. Kassim amesema tangu kuanza kutolewa kwa huduma hiyo ndani ya kipindi cha mwaka huu tayari wameshawafanyia upasuaji zaidi ya Wamama wajawazito 380 na wakamaliza salama kabisa pasipo tatizo lolote, Pia Waliojifungua kawaida ni zaidi ya 250 na wote kwa usalama , Aidha zaidi ya Watoto njiti 100 wamehudumiwa na Afya zao kuimalika salama kabisa.

(MCC) Chatanda amepongeza wato huduma wa hapo na kuwataka kuendelea kujitoa kwa moyo mmoja katika kuhudumia Afya za Watanzania.





TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments