DIWANI ALALAMIKA KUNYIMWA NAFASI YA NAIBU MEYA

Diwani wa Kata ya Mirongo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Hamidu Said anaye lalamikia kunyimwa nafasi ya Naibu Meya 
……………………. 

Diwani wa Kata ya Mirongo Wilaya ya Nyamagana Hamidu Said aliyeibuka kidedea katika uchaguzi wa nafasi ya  Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza uliofanyika Juni 21, 2023 amelalamika kunyimwa nafasi hiyo nakusema  hadi sasa haelewi kwanini alikatwa

Malalamiko hayo ameyatoa jana  Jumatano Novemba 15 wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kunyimwa nafasi ya Naibu Meya.

Amesema katika uchaguzi huo wagombea walikuwa ni watatu na kura zilipigwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza Diwani huyo alipata kura 10 na wapili akapata kura 10 na watatu akapata kura 4 awamu ya pili Hamidu Said aliibuka kidedea kwakupata kura 14 ambapo alimzidi mpinzani wake kura 4.

“Nashindwa kuelewa kabisa kwanini nimenyimwa nafasi hiyo na kupewa mpinzani wangu ambae alishika nafasi ya pili,kama kunautendaji ambao unaonekana nimefaya kinyume zipo kanuni za kuniadhibu kupitia Baraza la madiwani kwasababu pale kunakamati ya maadili”,amesema Said

Aidha, Said amewaomba viongozi wote walioko kwenye nafasi mbalimbali kutumia nafasi hizo vizuri bila kuwa na upendeleo wowote wala kubagua watu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments