Eriksen, Hojlund waumia

 


MANCHESTER, England: KIUNGO wa Manchester United, Christian Eriksen atakuwa atakosa michezo kadhaa kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.

Majeraha hayo huenda yakamuweka nje mchezaji huyo kwa mwezi mmoja, taarifa ya klabu hiyo imeeleza kupitia tovuti yao.

Mshambuliaji Rasmus Højlund pia anasumbuliwa na nyama za paja, United imeeleza huenda Hojlund akarejea mwishoni mwa mwezi huu.

Kikosi cha Ten Hag hivi karibuni kimewakosa majeruhi wachache wakiwemo Lisandro Martinez, Luke Shaw, Tyrell Malacia, Jonny Evans, Casemiro na Amad Diallo huku Aaron Wan-Bissaka akikosekana mechi dhidi ya Luton kutokana na kuugua.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments