Jkt Queens yachomoza Tuzo za CAF 2023


Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limemjumuisha Golikipa wa JKT Queens na timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars, Najiat Abbas kwenye orodha ya wanaowania tuzo ya kipa bora wa Afrika mwaka 2023.
Najiat ambaye alikuwa na kikosi cha JKT Queens katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake huko nchini Ivory Coast ni miongoni mwa makipa 10 wanaowania tuzo hiyo.
Katika hatua nyingine Winfrida Gerald wa Jkt Queens na timu za Taifa za wanawake amechaguliwa kushindania tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwenye tuzo hizo.
q
Kocha wa Jkt Queens Esta Chaburuma yupo pia kwenye kivumbi cha kusaka kocha bora wa mwaka kwa upande wa Wanawake , tuzo hizo zitatolewa Desemba 11, 2023 nchini Morocco.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments