Katibu Wa CCM,Dannel Chongolo Ajiuzulu,Wafanya Uteuzi Mkoa Na Wilaya.

Chama Cha Mapinduzi kimefanya kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa tarehe 29 Novemba 2023 Jijini Dar Es Salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan.  Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilijadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hapa nchini.

 
Aidha, kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kimefanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.
 
Nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa
Mkoa wa Arusha: Wanachama waliojitokeza 89, Walioteuliwa ni: -
1.    Ndugu Dkt. Daniel Mirisho PALLANGYO
2.    Ndugu Loy Thomas SABAYA
3.    Ndugu Solomon Olesendeka KIVUYO
4.    Ndugu Edna Israel KIVUYO
 
Mkoa wa Mbeya: Wanachama waliojitokeza 48, Walioteuliwa ni: -
1.    Ndugu Felix Jackson lYANIVA
2.    Ndugu Patrick Adkin MWALUNENGE
3.    Ndugu Fatuma Ismail KASENGA
 
Mkoa wa Mwanza: Wanachama waliojitokeza 109, Walioteuliwa ni: -
1.    Ndugu Michael Lushinge MASANJA (Smart)
2.    Ndugu Sabana Lushu SALINJA
3.    Ndugu Dkt. Anjelina William SAMIKE
4.    Ndugu Elizabeth Watson NYINGI
5.    Ndugu David Mayala MULONGO
 
Nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya
Wilaya ya Mpanda: Wanachama waliojitokeza 36, Walioteuliwa ni: -
1.    Ndugu Hamis Chande SOUD
2.    Ndugu Joseph Aniseth LWAMBA
3.    Ndugu Josephina Yusuph BARAGA
4.    Ndugu Emmanueli David MANAMBA
Wilaya ya Kusini Unguja: Wanachama waliojitokeza 15, Walioteuliwa ni: -
1.    Ndugu Maryam Suleiman HAJI
2.    Ndugu Ali Timamu HAJI
3.    Ndugu Mohammed Haji HASSAN
 
Kuhusu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwake, na ameridhia ombi hilo.
 
Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kimepongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments