Kikwete atoa wito kwa wajawazito

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa wajawazito kuhudhuria Kliniki kwa wakati ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto.

Kikwete ameyasema hayo Novemba 17, 2023 kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto aliyezaliwa kabla ya kukamilika wiki 37 za umri wa mimba ‘ Mtoto Njiti’ yenye kauli mbiu “Hatua kidogo, Faida kubwa, huduma ya Ngozi kwa Ngozi, kwa Kila Mtoto, kila mahali”
ambapo amesema wajawazito wakiwahi kliniki mapema watapata huduma na elimu stahiki.

“Naomba nitoe rai kwa wajawazito wote kwamba wahudhurie kliniki ipasavyo ili wapate elimu na huduma stahiki, wajifungulie kwenye vituo vya kutolea huduma na wahudhurie kliniki baada ya kujifungua, ” amesema.

Aidha, amepongeza jitihada zinazofanywa na Shirika lisilo la Kiserikali la Doris Mollel Foundation linalojihusisha na kusaidia watoto Njiti’ kwa kugawa vifaa tiba, kutoa elimu kwa umma kuhusu watoto njiti na kuhakikisha watoto njiti wanaishi katika mazingira bora.

Kikwete, pia ametoa wito kwa Serikali na wadau mbalimbali kuanzisha wodi kwa ajili ya watoto wachanga katika kila hospitali za Mikoa na Wilaya nchini.

 

“Naomba nirudie tena ushauri kwamba; mikoa, halmshauri na wadau, ihakikishe kuwa wodi za watoto kwa ajili ya huduma za Watoto wachanga (NCU) zinaanzishwa kwenye Hospital zote kama ilivyoelekezwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, R wakati wa uzinduzi wa takwimu za TDHS&MIS za 2022,” amesisitiza.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments