Makamu Mwenyekiti Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Abdulrahman Kinana, amewapongeza mabalozi wote wa jimbo la Rufiji kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa kwa Chama hicho kwa kusimamia Serikali inapotekeleza miradi ya maendeleo.
Kinana amesema hayo leo alıpozungumza na mabalozi zaidi ya 800 wa Jimbo la Rufufiji wakati Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa alipowaita kushiriki katika mkutano wa jimbo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa wananchi.
Ili kuharakisha Utatuzi wa Kero za wananchi, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewaagiza viongozi wa ngazi mbambali, waliochaguliwa na kuteuliwa kujenga utamaduni wa kuwatembelea mabalozi katika kata na mitaa, wawasikilize na kupata maoni yao.
“Mabalozi ndio wanaoishi na wananci kila siku, ndio wenye kujua furaha na huzuni zao, mabalozi ndio walioko katika maeneo ambayo miradi inatekelezwa na ndio wanaojua kama mradi unakwenda vizuri au hauendi.
“Mabalozi ni sikio la Chama, mabalozi wanasikia mengi sana mazuri yanayosemwa kuhusu Chama chetu, wanajua mazuri na kasoro za Chama na serikali yetu. Kwa hiyo ni muhimu tuwe na mawasiliano ya mara kwa mara,” alisema Kinana
Aliongeza kuwa hakuna sababu ya kuwa na mawasiliano na mabalozi wakati wa uchaguzi tu, ni vema mawasiliano yakadumishwa muda wote.
“Nichukue nafasi hii kuwaagiza viongozi wa Chama waliochaguliwa na walioteuliwa katika nafasi mbalimbali ndani ya Chama na serikalini kujenga utamaduni wa kukutana na mabalozi na kuwasikiliza.
"Tuwe na utamaduni wa kukutana na mabalozi, kama hatuwezi kuwakusanya hivi kama tulivyofanya leo nendeni katika kata zao, matawi yao na mitaa yao," amesema.
0 Comments